• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara Kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Manyoni District Council
Manyoni District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
      • History
        • Orodha Viongozi
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
      • Mchoro wa Kiutawala
      • Picha Ya Taasisi
    • Idara/Vitengo
      • Utawala & Utumishi
        • Majukumu ya Idara
        • Legal Seatings on Council's level
        • Department Information
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maji
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi & Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Utawala wa Mazingira na Usafi
      • Ujenzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio Vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
      • Huduma Zetu
        • Afya
        • Elimu
        • Maji
        • Kilimo
        • Mifugo
        • Uvuvi
    • Kilimo cha Korosho
    • Msimu wa mashamba ya Korosho 2019/2020
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha Ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba Ya Picha
    • Matokeo ya Kidato cha Pili 2018

Wazazi na Jamii watakiwa kushrikiana na Watumishi wa Serikali katika maendeleo ya Elimu

Imewekwa Mtandaoni mnamo: February 27th, 2020

Wazazi na jamii kwa ujumla katika Halmashauri ya Wilaya Manyoni  wameaswa kutambua kuwa suala Elimu siyo jukumu la Walimu na Watumishi wa Sekta ya Elimu peke yao bali ni la kila jamii Kushiriki katika kusimamia na kuboresha masuala mbalimbali ya kielimu ikiwemo kushauri namna bora za uendeshaji wa elimu.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Manyoni  Mh. Rahabu Mwagisa alipokuwa akifungua Mkutano wa Wadau wa Elimu wa Halmashauri ya wilaya ya Manyoni uliofanyika katika ukumbi wa  halmashauri  tarehe 27/2/2020.

Mwagisa amesema kuwa jukumu la Elimu ni la kila mmoja kwa nafasi yake kama  ambavyo Walaka wa Elimu namba 6 wa mwaka 2015 unavyofafanua.

Akitoa ufafanuzi  Mwagisa amesema kuwa waraka wa Elimu bila malipo una lengo la kuhakikisha kuwa kila mtoto wa kitanzania anapata Elimu. “Serikali ya awamu ya tano imepitisha walaka huu kwa lengo la kumsadia mzazi kumpunguzia majukumu  ili kuweza kumpa nafasi ya kumsomesha mtoto ili kila mtoto apate elimu ili iweze kumsaidia hapo badae” Alisema Mwaigisa.

Kuhusu  usimamizi wa elimu Mwagisa alisema kuwa kazi kubwa ya Serikali ni kuajiri na kulipa walimu mishahara ,kutengeneza sera na mtaala wa elimu, na kwamba walimu wana jukumu la kuwalea wanafunzi kwa kuwapa ujuzi ,maarifa kulingana na mtaala uliopo.

Mwagisa aliongeza kuwa Maafisa Elimu wanawajibu wa kusisimamia utekelezaji wa sera za elimu  wakati mzazi au mlezi wa Mwanafunzi ana jukumu la kuhakikisha anampatia mwanafunzi huduma zote kama vile kumpatia daftari,sare chakula na mahitaji mengine ya kila siku.

Akitoa rai kwa jamii Mwagissa amesema kuwa jamii  ihakikishe kuwa inakagua miundo mbinu yote inayozizunguka shule za wilaya ya manyoni, na kuhakikisha wanafunzi wanasoma katika mazingira na shule bora ,kuhakikisha miundombinu katika kila shule inaboreshwa ili kuweza kumfanya mtoto kuona maisha ya shule ni bora.

Akitaja jukumu la mwanafunzi Mwagisa amesema kuwa mwanafunzi anajukumu la kusoma kwa bidii kuheshimu sheria na taratibu za shule husika lakini piakuwa na heshima kubwa kwa kila mtu anaemzunguka na kwa walimu pia.

“kutokana na majukumu haya ndugu wajumbe na wanajamii mnaona ambavyo sasa suala la Elimu ni la kila mmoja na siyo la mtu mmoja tu hapa kila mtu anajukumu lake”amesema Mwagisa.

Mbali na Sera ya Elimu jamii imeaswa kupinga unyanyasaji wa kijinsia na ukatili kwa watoto kwani ili mtoto aendelee vizuri na kupata elimu na kuweza kuwa na uwezo mkubwa darasani ni lazima alindwe vema nakuepushwa katika vitendo vyovyote vinavyoweza kumpelekea kufeli,ama kukatisha ndoto zake kielimu. 

Mwagisa amewataka wanajamii kupaza sauti zao kupinga vikali unyanyasaji wa watoto na hasa watoto wa kike kwani amesema kuwa watoto wakike wanakatishwa masomo kwa makusudi na kulazimishwa kuolewa  ameitaka jamii ya wanamanyoni kupiga kelele juu ya vitendo vya kikatili vinayotendeka Wilayani humo.

Naye mbunge wa Manyoni Mashariki Mh. Daniel Mtuka ameiasa jamii kuonyesha ushirikiano kwa watendaji hasa walimu ikiwemo kutembelea mashuleni na kujua changamoto mbalimbali na ameliomba jeshi la Polisi kuhakikisha kuwa kesi dhidi ya unyanyasaji wa Watoto hususani wanafunzi zifuatiliwe na wanaobainika na makosa mbaimbali ya unyanyasaji ikiwemo ubakaji wafikishwe mahakamani ili iwe funzo kwa wote ambao wanafanya vitendo viovu na kuwasababisha Watoto kushindwa kuendelea na masomo.

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (CSEE) 2020 January 15, 2021
  • Matokeo ya upimaji wa kitaifa wa kidato cha pili (FTNA) 2020 January 15, 2021
  • Matokeo ya upimaji wa kitaifa wa Darasa la nne (SFNA) 2020 MANYONI January 15, 2021
  • JINSI YA KUPATA SHAMBA LA KOROSHO MSIMU WA 2019/2020 May 13, 2019
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • Waziri Lukuvi apiga marufuku viongozi wa Vijiji na Vitongoji kuuza ardhi

    January 11, 2021
  • TRC NA MIKAKATI YA UREJESHO WA HALI ZA MAISHA KATIKA MRADI WA SGR MANYONI

    December 23, 2020
  • Baraza lahimizwa kuweka kipaumbele katika Viwanda na uzalishaji wa Malighafi

    December 18, 2020
  • Naibu waziri wa kartiba na Sheria Mh. Geofrey Mizengo Pinda atembelea Manyoni.

    December 14, 2020
  • Angalia zote

Video

Ngoma za asili Siku ya UKIMWI Duniani
video zingine

Kurasa za Karibu

  • About Manyoni
  • Completed Projects
  • Ongoing Projects
  • Primary Schools Students Registration (Prem)
  • Instagram

Tovuti Mashuhuri

  • TAMISEMI
  • President's Office, Public Service Management
  • Singida Region
  • Necta
  • Kupata Salary Slip

Fuatiliaji ya watembezi wa Kidunia

world map hits counter

Kihesabia Watembezi

writingMasterThesis

Ramani

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni

    Sanduku la Posta: S.L.P 60, Manyoni

    Simu: +255 26 2540136

    Namba ya Simu: +255 712 028027

    Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera za Siri
    • Malalamiko
    • Maswali ya Mara Kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma

Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.